Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, October 9, 2015

MGOMBEA UBUNGE WA ARUSHA MJINI KWA TIKETI YA ACT-WAZALENDO AFARIKI DUNIA

Mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Estomih Malla amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC Moshi.

Marehemu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa tatizo la shinikizo la juu la damu.

Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo madaktari wa pale walisema Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.


Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba marehemu alifariki usiku wa kuamkia leo Oktoba 9, 2015 majira ya saa Saba.

ACT-Wazalendo kitatoa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huo baada ya kufanya mawasiliano na viongozi waandamizi wa mkoa na kitaifa.

Huyo ni mgombea wa tatu kufariki ndani ya siku 30 ambapo Septemba 12 mgombea ubunge wa jimbo la Lushoto kupitia CHADEMA Mohammed Mtoi alifariki dunia kwa ajali ya gari.

Septemba 24, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga kupitia chama cha Mapinduzi alifariki dunia nchini India alikokuwa anapatiwa matibabu

Uchaguzi wa ubunge jimbo la Arusha mjini utaahirishwa ili kutoa nafasi kwa chama cha ACT-Wazalendo kuteua mgombea mwingine.

No comments:

Post a Comment