Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, October 2, 2015

HALI YA MWANAMUZIKI NDANDAA KOSOVO SI SHWARI AUGUA NA KUTAPIKA DAMU


MWIMBAJI na rapa maarufu hapa nchini, Ndanda Kosovo hali yake si shwari na amelazwa hospitali kutokana na kupata maumivu ya tumbo yanayomsababishia kutapika damu.
 
 
Ndanda aliyetesa na bendi ya FM Academia na Stono Musica, amelazwa katika hospitali ya PKA iliyoko Tegeta jijini Dar es Salaam. 

Msanii huyo mcheshi ameimbia Saluti5 kwa njia ya simu kuwa amelazwa hapo tangu jana (Jumatano) ambapo tatizo kubwa ni kupasuka kwa mmoja ya mishipa tumboni. Ndanda amesema amekuwa akitapika damu, lakini madaktari wanajitahidi kudhibiti tatizo.





NA KUPITIA UKURASA WAKE WA FACE BOOK MWANAMUZIKI HUYO ALIANDIKA HIVI NA KUPOSTI PICHA HIZO

Bandeko bosambela pona nga depuis lobi nazo sanza makili
Ndungu zangu muniombeye natapika damu toka Jana usiku mungu anitanguliye.

mwisho wakunukuu.


KIKUBWA NACHOWEZA KUSEMA NI KWAMBA TUNAKUOMBE AUPONE HARAKA.

No comments:

Post a Comment