Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, October 31, 2012

SK ENTERTAINMENT INAKUAMBIA HAKIKISHA UNAICHEKI NGOMA MPYA YA KIDUM - KIMBIA NEW SONG 2012 NI HATARI




S.k Entertainment
kampuni ambayo imekuwa ikifanya kazi na mwanamuziki Jean piere Nyimbona aka kidum kibido tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 hapa bongo inakukaribisha kufuatilia ngoma mpya ya mwanamuziki kidum Kibido ambayo inaenda kwa jina la Kimbia hii ni ngoma kali sana na unakaribiswha kwa maoni pia na ushauri lakini pia kama ungehitaji kufanya show kwa hapa Nyumbani tanzania na mwanamuziki huyo tafadhali wasiliana na mi manager wake kwa hapa bongo ni Sophia Kessy Mmiliki halali wa SK Entertainment kwa email adress na namba za simu zinazopatikana hapo kwa kujua gharama na kufanya Booking ya show Mapema . Asanteni.

JINSI YA KUPIKA NYAMA YA BATA NA BIA

Mahitaji: Nyama ya bata gramu 500, pilipili hoho gramu 5, tangawizi gramu 10, vitunguu saumu gramu 5, bia chupa moja, chumvi gramu 8, sukari gramu 6, mchuzi wa sosi gramu 10, mafuta gramu 70, pilipili manga gramu 5, wanga gramu 5.   Njia ya kupika: 1. osha nyama ya bata, halafu uikate iwe vipande vipande, kata tangawizi na vitunguu saumu viwe vipande. 2. washa moto, halafu tia mafuta kwenye sufuria tia nyama ya bata, korogakoroga halafu tia vipande vya tangawizi, vitunguu maji, korogakoroga, halafu mimina bia na supu, baada ya kuchemka, tia chumvi, sukari na mvinyo wa kupikia na kupunguza moto, endelea kuchemsha kwa dakika 30, tia pilipili hoho na pilipili manga, halafu mimina maji ya wanga korogakoroga, na ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Ingabire ahukumiwa kifungo cha miaka 8 jela

Ingabire ahukumiwa kifungo cha miaka 8 jela Mahakama Kuu ya Rwanda imemhukumu mwanasiasa mkuu wa upinzani wa nchi hiyo kifungo cha miaka minane jela katika kesi inayohusiana na mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo mwaka 1994. Victoire Ingabire mkuu wa chama cha FDU-Inkingi ambacho kilikuwa hakijasajiliwa alikuwa akituhumiwa kwa makosa sita ambapo amepatikana na hatia na makosa mawili kati ya hayo yaliyotajwa.
 
Bi Ingabire amepatikana na hatia ya kula njama ya kuidhuru nchi kwa kutumia vita, kuzusha hofu na kukana mauaji ya kimbari yaliyotokea huko Rwanda.
 
Kwa upande wake mwanasiasa huyo wa upinzani nchini Rwanda amesema kuwa hana hatia.
 
 Watu zaidi ya laki nane waliuawa huko Rwanda wakati serikali ya nchi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na kabila la Wahutu na wanamgambo wa kabila hilo walipoanzisha mauaji yaliyodumu kwa siku 100, ambapo Watutsi na Wahutu wenye misimamo ya wastani waliuliwa.

Sandy Kimbunga chauwa 16 Marekani

FILE - In this Feb. 3, 2010 file photo, a sand hog works inside the massive cavern for the new 34th Street Station in New York that was carved out by giant tunnel boring machines. On Monday, July 23, 2012 the last of the 200-ton tunnel boring machines finished its mission digging 13 miles of new train tubes deep beneath New York City. The seven machine fleet bored through bedrock and created 16 new tunnels in 4 ½ years of digging. (Foto:Mary Altaffer, File/AP/dapd)
Idadi ya waliofariki dunia kutokana na Kimbunga kikubwa cha Sandy huko nchini Marekani imefikia 16 ambapo zaidi ya nusu ya vifo hivyo vimetokana na watu hao kuangukiwa na miti.
 
Vifo hivyo kwa ujumla wake vimeripotiwa katika majimbo ya New York, New Jersey, West Virginia, Connecticut, Pennsylvania na Maryland. Lakini kuna vifo vingine pia vimeripotiwa kutokana na kukatika kwa umeme na ajali ya gari katika balaa la kimbunga hicho.
Kuna ripoti ya mwanamke mwingine kufariki dunia kutokana na kimbunga hicho na mwili wake kuonekana ukielea katika maeneo ya bahari,huko Toronto nchini Canada jumapili. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha CNN Kimbunga hicho mpaka sasa kimeacha zaidi ya raia milioni 6.5 nchini Marekani pasipo nishati ya umeme katika eneo la Pwani ya Mashariki.


New York yaathirika zaidi
Vehicles are submerged on 14th Street near the Consolidated Edison power plant, Monday, Oct. 29, 2012, in New York. Sandy continued on its path Monday, as the storm forced the shutdown of mass transit, schools and financial markets, sending coastal residents fleeing, and threatening a dangerous mix of high winds and soaking rain.  (AP Photo/ John Minchillo) 
 
Jiji la New York
New York ni miongoni mwa mji ulivurugwa vibaya na kimbunga hicho ambacho rekodi zinaonesha kiliambatana na mawimbi ya urefu wa meta 4 katika eneo la kusini la Manhattan. Katika eneo hilo maji yalifurika mpaka katika njia kubwa kabisa ya reli. Na soko la hisa la New York limeendelea kufungwa kwa siku ya pili mfululizo.
Duru nyingine zinaeleza kwamba moto uliowaka usiku kucha umeteketeza takribani nyumba 50 katika kitongoji cha Queens. Taarifa hizo zimesambazwa na kitengo cha zimamoto kupitia ukurasa wake wa Twiter ambapo hata hivyo hakikutoa maelezo zaidi kufuatia mkasa huo. Lakini kama inavyofahamika kwamba mkasa huo umetokea baada ya kimbunga Sandy kuyakumba maeneo ya Pwani ya Mashariki ya Marekani ukiwemo mji wa New York.

Hata hivyo balaa la kimbunga hicho bado halijafika kikomo ambako wasiwasi bado upo katika maeneo ya mbali ya majimbo ya Wisconsin na Ilinois. Ishara ya tahadhari imetolewa kuanzia Chicago mpaka Maine na Canada mpaka Florida. Tahadhari hiyo inaonesha kimbunga Sandy kitaendelea kuwa tatizo katika siku kadhaa zijazo na kitaambatana na mvua kali, theluji na mafuriko.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP

HIKI NDICHO ALICHO KIANDIKA MBUNGE ZITTO KABWE KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK LEO

"Waziri wa Fedha amekubaliana na ombi langu la kufanya uchunguzi maalumu kuhusu fedha jumla ya tshs 25bn zilizochukuliwa na hazina kutoka Halmashauri zote nchini. Jibu la Serikali halikukidhi haja maana lilijibu mwaka wa fedha 2011/12 badala ya 2010/11. Kuna haja kubwa ya kuziba mianya ya ubadhirifu wa fedha za umma."

Tuesday, October 30, 2012

NATAKA KULEWA / DIAMOND

 
 


Wakimbizi wa Burundi nchini TZ warejeshwa makwao

 

Serikali ya Tanzania imeanza rasmi hatua za kuwarejesha makwao raia wa Burundi waliovuliwa hadhi ya ukimbizi.

Ni katika hatua za kuifunga rasmi kambi ya Mtabila ambayo ni kambi pekee iliyokuwa ikihifadhi wakimbizi wa Burundi nchini humo wapatao elfu thelathini na saba.
Shughuli ya kuwarejesha makwao kwa hiyari raia wa Burundi waliokuwa wakimbizi hadi mwezi Agosti mwaka huu kabla ya kuvuliwa hadhi ya ukimbizi na serikali ya Tanzania,ilimalizika rasmi Jumatatu ambapo kuanzia leo kinachofuata dhidi ya wakimbizi hao ni kuandikishwa kwa kufuatwa kwenye maeneo wanakoishi kambini na kisha kupakiwa kwenye magari na kurejeshwa Burundi.
Akizungumza na mwandishi wa BBC mjini Dar es Salam Eric David Nampesya, mkuu wa kambi hiyo ambaye ni mwakilishi wa wizara ya Mambo ya ndani nchini humo, Bwana Frederick Nisajile, alisema utaratibu huo utakavyokuwa baada ya kukamilika kwa shughuli ya kurejea kwa hiyari ya 'Kimombo Voluntary repatriarition.'
Bwana Nisajile alisema inatarajiwa kuwa raia wa Burundi wapatao elfu moja watarejeshwa makwao kila siku katika utaratibu huu ambao pia utawahusisha maafisa wa idara ya Uhamiaji ili kuwakamata wale wote watakaokaidi kurejea makwao.

kwa hisani ya BBC swahili.

Kiongozi wa upinzani Rwanda ahukumiwa jela


Victoire Ingabire
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire amehukumiwa miaka minane gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kosa la uhaini
Viongozi wa mashtaka walitaka afungwe maisha jela kwa kutishia usalama wa nchi.
Mahakama imempata na hatia ya kupuuza mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994.
Ingabire hakuwa mahakamani wakati hukumu ilipotolewa dhidi yake kwani amekuwa akisusia kuhudhuria vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo akisema imeshinikizwa ksiasa,.
Alikamatwa mwezi Aprili mwaka 2010 na kuzuiwa kushiriki uchaguzi uliofanyika mwaka huo.

kwa hisani ya BBC swahili.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Luten Mstaaf Chiku Galawa amezindua mashindano ya kitaifa ya michezo ya Kitaifa ya mpira wa kikapu

MKUU wa Mkoa wa Tanga Luten Mstaaf Chiku Galawa amezindua mashindano ya kitaifa ya michezo ya Kitaifa ya mpira wa kikapu ambapo pamoja na mambo mengine amewakata wananchi kuudhamini mchezo huo kama ilivyo katika mchezo wa soka.
Akizungumza na wanamichezo hao kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini pamoja na Mambo mengine mkuu huyo wa Mkoa amewaasa wanamichezo kuwachagua viongozi wa michezo wenye uwezo wa kuimarisha mchezo huo na ambao hawatafanyakazi kwa maslahi yao binafsi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na timu zilizoshiriki katika mashindano hayo Katibu Mkuu wa Mpira wa Kikapu Alexernder Msoffe amesema timu nyingi zimeshindwa kushiriki katika michuano hiyo kutokana na tatizo la uhaba wa fedha.
Michuano hiyo itachukua muda wa juma moja na timu 22 kutoka mikoa 11 hapa nchini zimeshiriki.

Jela miaka 25 kwa 'juju' na ulanguzi


Osezua Osolase

Mwanaume aliyewafanyia vitendo vya kishirikina au ''Juju'' wasichana ambao alikuwa anawalangua kutoka nchini Nigeria hadi barani Ulaya amehukumiwa jela miaka 20 nchini Uingereza.
Osezua Osolase raia wa Nigeria na mwenye umri wa miaka 42,kutoka mtaa wa Gravesend, Kent aliwatumia wasichana maskini kwa kuwahadaa kuwa wangepata maisha mazuri baada ya kufika alikokuwa anawapeleka.
Osolase alipatikana na hatia ya makosa matano ikiwemo ubakaji na kumfanyia dhulma za kingono mtoto mdogo.
Jopo la majaji lilisikia katika kesi hii iliyoisha siku ya Ijumaa kuwa vitendo vya kishirikina pia vilitumiwa kuwatia hofu waathiriwa watatu wa vitendo vya Osolase.
Jaji alisema kuwa Osolase ambaye ni mwathiriwa wa HIV, aliwatia hofu waathiriwa wake ili kuwalazimisha kumtii na kukaa kimya.
"umetenda dhulma na kuwafanyia unyama waathiriwa vitendo vyako'' jaji alimwambia bwana Osolase.
"wewe sio mwaminifu hata kidogo. Una kiburi na ukatili, hauna ubinadamu wala huruma kwa waathiriwa wako.'' aliongeza jaji
Aidha jaji Williams alisema kuwa bwana Osolase aliwaharibu wasichana hao wakati alijua kuwa ana virusi vya HIV na hata kumbaka msichana mmoja wakati akijua alifanya kitendo kibaya sana .
Osolase aliwapeleka wasichana hao kwake nyumbani kabla ya kuwapeleka barani Ulaya kufanya kazi ya ukahaba.
Mahakama ilisema kuwa mwanaume huyo arejeshwa nyumbani Nigeria atakapomaliza kuhudumia kifungo chake.
Mmoja wa wasichana alielezea yaliyomkuba wakati akifanyiwa vitendo vya kishirikina, alisema alitolewa damu mwilini , kisha akakatwa nywele zake za kichwani na sehemu zake za siri.Baada ya hapo alilishwa kiapo kutosema chochote.
Osolase alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Stansted mwezi Aprili alipojaribu kupanda ndege mwaka jana.
kwa hisani ya BBC swahili.

Zuma na Motlanthe wakosoana hadharani

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na makamu wake Kgalema Motlanthe wamekosoana hadharani mbele ya wanahabari jambo lililoonyesha kuwepo vita vya kung'ang'ania madaraka ndani ya chama tawala nchini humo ANC.

Mapema Makamu wa Rais wa Afrika Kusini alikuwa amesema kwamba nchi iko katika hali ngumu na kwamba uchumi umesimama.

 Baadaye Rais Zuma amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kusema matamshi ya makamu wake hayaakisi ukweli wa mambo kwani uchumi unasonga mbele na unakua kila siku.

 Hii ni katika hali ambayo viongozi hao wanatarajiwa kuchuana kwenye uchaguzi wa chama baadaye mwaka huu.

 Montlanthe amesema chama cha ANC kinahitaji mabadiliko kwani uongozi wa sasa umepoteza dira na kwa kiwango kikubwa umeitumbukiza nchi pabaya.

Rais Zuma amekasirishwa na matamshi hayo na kusisitiza kuwa huo si msimamo rasmi wa serikali.

Kimbunga cha Sandy chazidisha maafa USA

Kimbunga kikali mno cha Sandy kilichoanza kuikumba miji mbalimbali muhimu ya Marekani kinaendelea kusababisha maafa makubwa nchini humo.

 Zaidi ya watu milioni 6.5 hawana huduma za umeme katika majimbo ya pwani ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Watu wasiopungua 12 wameaga dunia hadi sasa kutokana na kimbunga hicho kikali. Upepo mkali na mvua kubwa zinazonyesha sambamba na kimbunga hicho zinatabiriwa kuathiri maeneo mengi ya kaskazini mashariki mwa Marekani.

 Kimbunga cha Sandy kimesababisha pia hasara ya mabilioni ya dola nchini humo. Vituo vingi vya treni vimejaa maji, maelfu ya safari za ndege zimevunjwa, mamia ya maelfu ya watu wameondolewa katika maeneo mbalimbali ili kueupusha maafa na matatizo mengine mengi.

Bondia wa TZ kuzipiga Afghanistan


Hamid Rahimi atatoana jasho na mtanzania Said Mbelwa.

Afghanistan inaandaa pigano la kwanza la ndondi kuwahi kufanyika nchini humo huku kukiwa na ulinzi mkali sana.

Masumbwi hayo yanayohusisha wanamasumbwi wa uzani wa middle, yenye kauli mbiu ya ''kupigania amani'' yatapeperushwa moja kwa moja kupitia televisheni.

Mamilioni ya waafghanistan wanatarajiwa kutizama mchuano huo kati ya bingwa wa ndondi nchini Afghanistan, Hamid Rahimi, na mshindani wake kutoka Tanzania, Said Mbelwa.
Ndondi ziliharamishwa nchini Afghanistan mwishoni mwa utawala wa Taliban.

kwa hisani ya BBC swahili.

Kimbunga Sandy chatikisa Marekani watu takriban milioni 50 kukosa makazi


Kimbunga Sandy kilianza kupiga kutoka nchini Cuba wiki iliyopita ambako ilisababisha vifo vya watu karibia ishirini


Maafisa katika idara ya hewa nchini Marekani wamesema takriban watu milioni hamsini wataathiriwa na kimbunga hicho

Mbinu mpya ya bei nafuu kupima HIV



Ikiwa mtu anavirusi rangu ya kifaa inabadilika kuwa buluu na ikiwa hana rangi unakuwa nyekundu
Aina mpya mbinu ya kuchunguza na kuona hata viwango vya chini vya virusi na hata aina ya saratani imezinduliwa na watafiti nchini Uingereza.
Utafiti huo unahusu majimaji ambayo hubadilika rangi kuonyesha ikiwa mtu ameathirika au la.
Aidha watafiti wansema mbinu hii mpya ambayo inahitaji utafiti zaidi, inaweza kuelezea kwa kina aina ya ugonjwa au virusi mfano proteni inayopatikana kwenye kirusi cha HIV.
Ikiwa dalili ya kirusi au ugonjwa ipo katika matokeo ya uchunguzi, basi inabadili rangi ya kemikali. Matokeo yatakuwa rangi ya buluu ikiwa kirusi kipo na nyekundu ikiwa kirusi au ugonjwa haupo.
Watafiti wanasema kuwa matokeo ya uchunguzu au upimaji pia yatapatikana mara moja.
Profesa Molly Stevens aliambia BBC: " Mbinu hii ya kupima magonjwa inatumiwa kuchunguzwa virusi hata kama ni vya viwango vya chini mno na kuongeza nafasi ya kuona ikiwa ugonjwa upo kwenye mwili wa mtu au la.

Hiki ni kifaa ambacho mtu anaweza kujipima mwenyewe hali yake ya HIV akiwa nyumbani
"Kwa mfano, ni muhimu kuchunguza viini vya ugonjwa vilivyo na viwango vya chini sana vya mfano saratani kwa mtu aliwahi kutibiwa ugonjwa huo kuona ikiwa saratani hiyo itaweza kuibuka tena hata baada ya kutibiwa."
"pia inaweza kusaidia katika kupima wagonjwa wa HIV, ambao viwango vya virusi viko chini sana kiasi cha kutoweza kuonekana kwa mbinu za sasa."
Watu waliopimwa mapema kutumia mbinu hii ya rangi, walionyesha dalili za HIV na saratani ya tezi ya kibofu, ingawa utafiti wake katika nyanja za juu bado utahitajika kabla ya kutumika hospitalini.
Watafiti wanasema kuwa wanatarajia kuwa gharama ya kifaa hicho itakuwa ndogo mara kumi kuliko mbinu za sasa za kupima magonjwa na kwamba itanufaisha watu katika nchi ambazo mbinu zilizopo hawawezi kuzimudu. Na pia itaweza kutumika sana katika kupima virusi vya HIV katika nchi maskini duniani.

Monday, October 29, 2012

PICHA ZAIDI MATUKIO YA HARUSI YA ANOLD KAYANDA NA MKEWE ANITHA.


















MKUU WA WILAYA YA KIBAHA AKEMEA VIJANA JUU YA MAKUNDI‏

MKUU wa Wilaya ya kibaha,mkoani Pwani Halima Kihemba amekemea tabia ya vijana ambao wanajiingiza katika makundi ya kihuni ambayo hayana tija yoyote na  yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na kujichukulia sheria mikononi.

Kihemba amekemea hali hiyo wakati alipokuwa akizungumza na  na viongozi na vijana wa Wilaya ya kibaha ambao wanatarajiwa kuanza kujiandaa kwa ajili ya kuanza  mafunzo ya ujasilimali,ambapo amesema anachukizwa sana na  vijana wenye jazba ambao wamekuwa wakivamia hata vituo vya polisi na kureta vurugu.

Pia Kihemba pia ametoa wito kwa wazee wa Wilaya ya kibaha kuhakikisha kwamba wanaisaidia serikali yao  katika kuwaelimisha vijaa kuachana na mwenendo wa kujiingiza katika makundi mabaya yamekuwa ni moja ya chanzo cha kuleta mogogoro.

NA MWANDISHI VICTOR KUTOKA KIBAHA.

RAIS KIKWETE AANZA ZIARA YA MKOA WA KILIMANJARO‏



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi mbalimbali na wananchi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro leo Oktoba 28, 2012 tayari kuanza ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same.






Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika uwanja wa stendi ya Same Kuhutubia mkutano wa hadhara leo Oktoba 28, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE - ZIARA YA KILIMANJARO‏


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JK: Moto wa dini hautakuwa na mshindi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumapili, Oktoba 28, 2012, ameanza ziara ya siku nne kukagua shughuli na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwaambia Watanzania kuwa moto wa dini ambao umeanza kujitokeza katika Tanzania hautakuwa na mshindi.
Rais Kikwete ameanzia ziara yake kwenye Wilaya ya Same ambako amehutubia mkutano wa hadhara kwenye eneo la Stendi ya Mabasi ya mjini Same ambapo amewaambia mamia ya wananchi kuwa baada ya watu wasioitakia Tanzania mema kushindwa kuwafarakanisha Watanzania kwa kutumia ukabila sasa wamegeukia dini.
“Kuna watu hawana raha na utulivu na amani ya nchi yetu. Walijaribu kutufarakanisha kwa kutumia ukabila lakini hili lilishindikana na sasa wamegeukia dini. Lakini ndugu zangu moto wa dini hautakuwa na wa kuuzima na hautakuwa na mshindi,” Rais Kikwete amewaambia wananchi kwenye mkutano huo.


Amewataka Watanzania kuendelea na utulivu wao wa kidini na wakatae kufarakanishwa kwa tofauti za dini. “Ndugu zangu, siku zote tumekuwa na dini zetu, kila mmoja akiwa na uhuru wake wa kuabudu anachokitaka na kukiamini na kwa namna anavyotaka yeye. Ni muhimu tuendelee kuheshimu tofauti zetu za dini bila kuzigeuza tofauti hizo kuwa chimbuko na sababu ya ugomvi.”
Rais Kikwete pia amewahakikishia wananchi wa Same kuwa Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji katika maeneo ya wilaya hiyo na wilaya za jirani za Mwanga na Korogwe katika Mkoa wa Tanga.
Amesema kuwa mradi mkubwa wa kusambaza maji katika vijiji 34 katika wilaya hizo kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu utaanza kutekelezwa Februari mwakani. Mradi huo wenye thamani za dola za Marekani bilioni 34 utawahudumia wananchi katika vijiji 14 vya Wilaya ya Same na utachukua kiasi cha miezi 18 kukamilika.
“Tutalifanya suala hili la ukosefu wa maji kuwa historia katika Wilaya ya Same. Baada ya miezi 18 kuanzia Februari mwakani tutakuwa hatuzungumzi tena tatizo hilo,” amesisitiza Rais Kikwete huku akishangiliwa sana na wananchi hao.
Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa mradi mdogo wa kutoa maji ya dharura katika Wilaya ya Same utaanza kutekelezwa wiki ijayo wakati pampu za maji zitakapoletwa kwa ajili ya kufungwa.
Rais Kikwete ataendelea na ziara yake leo, Jumatatu, Oktoba 29, 2012 kwa kuzindua Kiwanda cha Tangawizi kilichoko Mamba Miamba na kufanya mkutano hadhara na wananchi.

Baadaye kesho, Rais Kikwete atazindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Asha-Rose Migiro iliyoko Mwanga.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Oktoba, 2012

KIJANA WA JAHAZI LA CLOUDS FM ARNOLD KAYANDA NA ANITHA WAFUNGA PINGU ZA MAISHA


 Mtangazaji wa Kipindi cha Jahazi ndani ya Radio Clouds FM, Arnold Kayanda akiwa pamoja na mke wake Anitha wakati wakiingia kwenye hafla ya Ndoa yao iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karemjee, jijini Dar es Salaam.
 Bw. Arnold Kayanda na Bi. Aneth Kayanga wakilishana keki.
 Maharusi wakikata keki.
PICHA KWA HISANI YA KAJUNA SON

WANACHAMA WA UMOJA WA VIJANA CCM UV-CCM WATWANGANA NGUMI

 

Wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), wakiwa wamesimama na mabango makao makuu ya umoja wa vijana ccm kumpinga   kwa  Mwenyekiti mpya wa Taifa wa Umoja huo, Khamis Sadifa Juma na viongozi wenzake,  wakati alipowasili  makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam , akitokea mkoani Dodoma alipochaguliwa kushika nyadhifa hiyo.
Mwanacha wa (UV-CCM) katikati akiwa amekamatwa na wanachama wenzie kwa tuhuma za kupinga kwa mwekiti mpya 
Mmoja wa wanachama (UV-CCM)akipata kichapo kutoka kwa wanachama wenzake 

PICHA NA PHILEMON SOLOMON

JACK WOLPER ATWAA TAJI LA IJUMAA SEXIEST GIRL

Jacqueline Wolper (kulia), akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa DK. Cheni aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo.
Wolper akiwa ameshikiria cheti chake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi.
Dok. Cheni akiwa kwenye pozi na Wolper juu ya jukwaa.
picha za matukio haya ni kwa hisani ya kajuna son . Thank you bro