Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, April 27, 2012

KAMATI KUU YA CCM YARIDHIA KUVUNJWA BARAZA LA MAWAZIRI.




Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM iliyoketi leo Jijini Dar es Salaam imeridhia uamuzi wa Mwenyekiti wake Rais JAKAYA KIKWETE kuvunja na kulisuka upya Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

 
Uamuzi huo wa Rais KIKWETE wa kuliunda upya Baraza hilo umekuja baada ya kupokea taarifa ya maazimio ya Kamati ya Wabunge wa CCM iliyoketi Mjini Dodoma wakati wa vikao vya mkutano wa saba wa bunge uliomalizika hivi karibuni.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa NAPE NNAUYE ameeleza kuwa pamoja na Kamati Kuu kuridhia uamuzi wa Rais KIKWETE pia imemtaka awawajibishe watendaji wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali ambao wamehusika katika ubadhirifu wa mali na rasilimali za umma.

Katika hatua nyingine Kamati Kuu imeipongeza Kamati teule ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa ripoti yao ya uchunguzi  iliyobaini  ubadhirifu katika baadhi ya sekta ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment